September 8, 2025
CN
Don Birhange
September 8, 2025

6IXVIEWSII8K MIXTAPE REVIEW

Card Image
Share

Album: 6ixviewsii8k

Artist: Boutross

Genre: Shrap

Year: 2020

Ukisorora design yenye Bouti siku hizi anapiga collab hadi na mastar kaa Konshens, inabidi tu umemtii. But pia haijakuom virahisi. Ilibidi amechapa wera videadly ndio afike penye ako sahii.

Mara ya kwanza kusikia Boutross ilikuwa huko ma 2017, kwa ngoma ya Octo wakiwa na Barak Jacuzzi inaitwa ‘Tergat Gang’, na instantly, nikafeel huyu jamaa atakuwa mnoma. Baadaye alirelease mixtape inaitwa ‘Billy Jean’, alafu tena akatoa ‘Turn a Hobby to a Job’ na mamorio wake wa AD Family; kina Jovie Jovv na Kay Green. Ngoma yao ya ‘Juice Man’ ikahit videadly hadi wakafanya remix na Sho Madjozi wa SA.

Akianza, Boutross alikuwa anapenda kuroga more na kilami na kuingiza sheng kiasi, lakini by the time tulingia 2019, alikuwa ameadisia sheng mob kwa mangoma na hapo sasa ndio Shrap ikaanza kutamba. Alidrop masingle kama ‘Safi’, ‘Wrong’, ‘Omoka’ na ‘Wasoro’, zote zikakuwa mabanger kuruka. Saa akaanza kujulikana zaidi kwa industry na mafans wakakuwa wengi. So ni ile wadhii wanangoja Shrapgod adrop project ingine na wanaexpect ikuwe moto mbaya.

Hapo magithaa ya February 2020, finally, akadrop ‘6ixviewsii8k’ na wallahi iliweza! Alikuwa ameseti mixture ya RnB, Pop, Trap na Shrap. Alafu alikuwa na macollab na wasanii kibao ungedhani ni Avengers wameassemble. Hata hivyo, bado mangoma zilikuwa na vibe tifi na beats wazimu.

Ngoma ya kwanza inaitwa Toa. Hapa maze anakatia tu ngeus, so unakiche inakushika offguard juu hatukuwa tumemzoea akiimba. Anasema vitu kama “chemsha bongo chemsha lolo” unajua tu jamaa ako kutu kuliko Titanic, anadai kuhanya ka panya.

Ya pili ni Pendeka, yenye alicollab na Xenia Manasseh alafu Zikki akaimba chorus. Bouti anakatiana akidai vile atafanyia manzi ‘acrobatics’. Manasseh naye, mwenye sauti yake inaweza fanya shughuli zote zisimame tao, anasema tu vile anadoubt na hadai kuvunjwa roho. Ngoma nare sana.

Sa ya tatu ni Fell in Love. Afrobeats zimetulia na hapa enyewe unaweza dhani jamaa amepata Cinderella wake juu ya vile anamwimbia vile ametekwa na anamdai ile crazy. Shida ni huyu ngoko anapenda wathii wako na mkwanja mob lakini bado anajaribu kumchipo. Mwanaume ni effort ama aje?

Ngoma ya nne nayo ni Chorea na inatake place kwa klabu. Anaongelea tu vile madem hufuata masponyo na vile mandume wengine ukiwacheki unajua tu hawadai zogo. “Cheki anavyoekelea itabidi manzi ameekelewa”. Sa hapa anasema vile anarombosewa hakuna vile hiyo reba itaisha kwa dance floor, lazima further negotiations vile Fabrizio husema.

After hiyo, next inaitwa Friend Zone. “She told me pull up at the bando, I know I’m about to hit it, Then she put me in the friendzone, Why you do this mamacita”. Sa huskii hapa Bouti alikuwa akilink na dem lakini akamdedi na dem hayuko ithaa. Sa vile dem anaanza kumdai yeye pia anaamua kumdodge. So situation hapa imekuwa tu toxic, madrama tu.

Song ya sita inaitwa Sin Thea na iko na Nviiri The Storyteller. Hapa morio wetu amelearn madem wanaeza kumaliza juu amevunjwa roho so hadai story zao. Nviiri naye ako za “You made a heartbreaker not a lovemaker, tangu uhepe siku hizi nateka”. Unacheki ile design ukivunjwa roho pia wewe unaanza kutojali, unakuwa mtu kazi mapenzi kando, sa ndio anaongelea kwa verse yake.

Ya saba inaitwa Juju. Labda bado kuna hope juu hapa ametekwa na mpoa mshifre mbaya so ni ile ako za ni kaa amepewa love potion. Hii iko na vibe imetulia ngoma fiti ya kuimbia msupa. Stuff ingine ni ati kwa hii ngoma alisample ngoma ya Nameless na Mr Lenny yenye pia inaitwa Juju lakini hiyo iko na vibe ya kapuka. Hadi kuna part anasema “Nikikuona nashikwa na kifafa, naanza kuropokwa” kama ngoma orijee.

Song ya nane nayo inaitwa Soul na ako na Shappaman. Ngoma fiti ya kuskiza ukimedi ama ukiseti kimoja. Sa hapa ndio tunaanza kuona Shrap maze, inaanza akisema “Shida ni sinanga patience na shawty anapendanga attention” Sa hapa tushajua riomo amekuwa mtoxic. Sa stuff hunimada ni ati anasema “Stori huanza na kitu safi kwanza mlipatana Pizza Inn mdomo inatoa tu mavi madam itabidi ucheze na Listerine” Ebu imagine we ni dem umeenda date alafu kitu ya kwanza unaambiwa ni hii? Ngori maze.

After hiyo ni Us na iko na Kristoff, Dope-I-Mean na Ex-Ray. Sasa hii ni club banger moja hatari inapraise wasupa wamebeba hapo nyuma ka kilogram salas, design wanaweza tingisha nyumba ki-Julius Malema. Si mnajua nyash ni national asset si swali. Kuna bar moja kali ya Kristoff hunibamba “Mi ni mluhya hawa madem mi huwakunywa ka chai”. Na hiyo time Gengetone ilikuwa form so of course unajua Ex-Ray aliua verse yake.

Track ya kumi inaitwa Tiga Urimu yenye inamaanisha ‘wacha ujinga’. Iko na kisapere mob lakini ni ngoma noma excess (si bado nyi huskiza mareggaeton na si ati mnarada, bora mnaifeel). Ngoma kaa hii ukicheza kwa roadtrip, vaibu tupu! Sa Kay J anadai ati vile amefall in love na “gutire gushonoka” yaani yeye hana aibu anadai hiyo mapenzi. Bouti naye haamini story za mapenzi anajua atachezwa (anadai tu kutinga mali) lakini Raj ye ni ka lover boy ako za “Nitakulinda honey kama nyuki, wachana na hawa mahaters wana chuki”.

Sasa after kusample ngoma yake, akafanya feature na none other than Nameless mwenyewe inaitwa Band Wagon. Hii ngoma basically wanaongelea vile wamecome up from kuwa maunderdogs wakakuwa mastar.

Take me Whole ndio the twelfth track. Sa hapa kuna njia mob ya kuinterpret but ile niliona ni ni kama anaplead na toto akuwe na yeye juu ako madly in love. “I cannot see, loving you makes me violent she took my sight yeah she blind me”.

After hapo sasa, ni shrap na trap tupu, ukisikiza na debe, zinachuna mbaya unaweza geuka kiziwi. Of course, lazima angeanza na ile ngoma ya umati Story Ilianza. Hii nayo reba iliflow vifiti excess. I doubt kuna msee hajui hii ngoma. Basically anaongelea design madem wa club huteka wasee alafu wanawatoka kila kitu. Mchele si ya pishori maze avoid. Kujichunga ukiwa dunda muhimu.

Ngoma next nayo iko na maheavyweight wa drill huku 254, Zozanation yenyewe, Wakadinali (Domani na Scar) na Mastar VK “Buda juu nimeomoka nikipita kwa njia ondoka”. Sa kwa Omoka, wanaringa tu vile dooh imewapea maisha smart. Mastar VK husema hadi “Juu shoti napiga kwa chweza buda ju nimeomoka, na fare silipangi chweza, Uber juu nimeomoka” unacheki vile ameleta hiyo rhyme vifiti hadi unatii tu.

Wasoro ni wasee hudai kuingilia riba za kila msee. Kwa hii track, anaongelea vile tu wathii walidoubt shrap lakini sasa imeboom ikakuwa kitu kubwa hadi wao hawawezi ignore.

Next ni Rieng, na hii ngoma ni fiti ya kusikiza ukiwa umechill na mariomo mkiwa zabe. Hii pia yeye aliroga na wasee wa AD Familia Kay Green na Dope-I-Mean, wanadai vile hawatense msee. Alafu si unajua mamorio wakichill area jamo, reba za kuzama kwa ziwa haziwezi kosa.

Ngoma inafuata inaitwa Bank na ameimba na Barak Jacuzzi. Jamaa huroroa ngoso unaweza dhani ni wa Atlanta, Georgia lakini kumbe ako Nyeri; sa huskii ganji ni cheddar, geri ni gang, Trapanese huwa lugha ngori.

After hapo tunatoka Atlanta kama tumeingia Colombia kiasi, track inaitwa Coca na Medica. Iko na hook lazy na trap vibe imetulia. Hadi ilifika part “My nigga just wanna geek” inarudiwa mara mob na sauti ka ya mjunior karibu nidhani Playboi Carti amekuwa featured.

Hit that Whoa huwa na 808s zingine mwenda ukisikiza kwa nganya ya Ronga hata unaweza kosa kusikia donda akisema umefika pahali unaenda. Trap moja fisa sana na flow hatari.

Ngoma ya mbaula, Safi, sa ndo waliamua wanaroga kama wamekuwa wachawi wa movie za Naija. Bouti huanza akiongelea vile ye ni mzii kwa industry, hepi na kuwa na madem kibao. Alafu anacheza ka De Bruyne kwa Haaland na Asum humaliza beat completely. Inasemekana ukipitia huko LA kwa makaburi utapata kaburi ya hiyo beat juu waliimada na kuizika na flow hatari. Sijawahi confirm lakini, mkiipata mnichanue.

Next inaitwa Cute akiwa na Dope-I-Mean wanaongelea tu mashpleng na vile wao huteka mabaddie videadly.

Najua labda unashangaa huyu jamaa hajasema ata ile ngoma anapenda sana. Sasa hii next hata ukiniamsha saa nane usiku naweza imba yote. Inaitwa Mbona, na wallahi nakushow nikisikia Boutrosss amesema “Mi huingia base naitinga geri haijali makali mapinga”, mi huroga ka chizi. Hii ngoma yote anajigamba na vile ameearn right ya kujido na kuwa mauru kiasi. Line napenda excess ni akisema “Juu ya mahali nimetoka kurudi sidhani I’m able, so ukishika makali utanyongwa Bouti anazidi kusonga”. Na in short hapa anashow wasee wasitense kujinice na wameearn it, usijali hata vile wasee wataongea juu “Mbona you mad?

Ngoma next huitwa Yengs ako na Mastar VK wakidai vile wako na wasupa kibao na si ati madem wameraka, ni manyanga kuruka. Na of course wamebeba hadi Bouti husema “Dem alikalia boy kwa uso, boy akastop the breathing” yaani huyo yut akakuwa assmatic, unacheki.

Ya mwisho inaitwa Chase na ako na TNT. Hapa ni tu vile madem hupenda kusukwa “Shawty aliringa na meow mpaka alinicheki vvip kiti”, lakini si mnajua hakuna mkate ngumu mbele ya chai. Alafu si unajua lazima wataflex dooh “Nacheza na dose, Bouti allergic to broke niggas

So hapo ndio album iliisha na sidhani kuna wasanii wengi wanaweza sema wako na album zimejaa mahit kaa hii. Boutross ako na talent wazimu na niko sure ataendelea kutupea mangoma wazimu for the span of his career.

______________________________________________________________________________

Don Birhange is a music enthusiast who enjoys listening to and discussing various genres. Dive into his Spotify playlists & Mixcloud mixes to get a feel of what he's about!

To communicate with the writer, find him on:

Email: tbirhange@gmail.com

Instagram: tbirhange

To listen to his playlists and music, find him on:

Spotify: Don Birhange

Mixcloud: Flarefadaze

Leave a comment

Loading comments...
Card Image
Don Birhange
CONTRIBUTOR

Don Birhange is a music enthusiast who enjoys listening to and discussing various genres. Dive into his Spotify playlists & Mixcloud mixes to get a feel of what he's about! To communicate with the writer, find him on: Email: tbirhange@gmail.com Instagram: tbirhange To listen to his playlists and music, find him on: Spotify: Don Birhange Mixcloud: Flarefadaze

Join Community

Step into Qwanis vibrant circle of creatives. Here, every voice matters, every story thrives, and camaraderie blooms. Become a part of our literary mosaic today!

View Our Events
Pens

© 2025 Qwani. All rights reserved. Designed by Qwani. Powered by Chari Designs